DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, March 28, 2014

MATUKIO YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA YALIVYOFANA DODOMA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa serikali na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dodoma muda mfupi mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani humo hivi karibuni.

Wanafunzi wametambua umuhimu wa maji na rasilimali zake hivyo waliitikia wito na kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani Dodoma hivi karibuni.

Baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa baadhi ya  vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dodoma wakipata ufafanuzi juu ya pampu za kuvuta na kusukuma maji. Elimu juu ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya maji, uhifadhi na utunzaji vyanzo na rasilimali za maji zilitolewa kwa wingi kwenye maadhimisho hayo yaliyoambatana na maonesho ya huduma za maji kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Teknolojia rahisi ya uvunaji maji ya mvua kwenye majengo/makazi yetu ni moja kati ya elimu iliyowavutia wananchi wengi wakati wote wa maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani Dodoma yaliyoambatana na maonesho ya huduma za maji kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma hivi karibuni.

Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ( nyuma mwenye miwani) akiwa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani dDodoma wakishangilia kuhitimishwa kwa maadhimisho ya wiki ya Maji kitaifa mkoani Dodoma hivi karibuni, wanafunzi walionesha kuelewa umuhimu wa vyanzo na rasilimali za maji kwa jamii.

No comments:

Post a Comment