RC DODOMA DR. REHEMA NCHIMBI AKAGUA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA NHC KONGWA
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Alfred Msovella akimuongoza Mkuu wa Mkoa Dodoma
Dr. Rehema Nchimbi wakati akikagua ujenzi wa ndani wa nyumba za shirika la nyumba
la Taifa unaotekelezwa Wilayani Kongwa. Jumla ya nyumba 44 zenye mchanganyiko
wa vyumba viwili na nyingine vitatu zinatarajiwa kukamilika Aprili 2014 na
kuuzwa kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliosimama mbele)
akiwa na viongozi wa Wilaya ya Kongwa na wataalamu wa ujenzi wa NHC wakifanya
majumuisho mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba 44 za shirika la
nyumba wilayani Kongwa.
Baadhi ya nyumba za shirika la nyumba la Taifa zinazojengwa eneo la
Mnyakongo kwenye mji wa Kongwa, mradi huo una jumla ya nyumba 44 ambapo ujenzi
wake umefikia asilimia 80, zitakamilika mwezi April 2014 na kuuzwa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment