RAIS Jakaya Kikwete (pichani), leo atapokea ‘Katiba
Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel
Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri
mjini Dodoma.
Bunge
hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya Katiba
mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya
Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha Katiba inayopendekezwa
iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.
Katiba
hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka
vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama
tawala, kitendo ambacho kiliibua mjadala kwa taifa zima huku makundi mbalimbali
yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga. |
No comments:
Post a Comment