DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, October 08, 2014

OMMY DIMPOZ KUSINDIKIZA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2014 JUMAMOSI HII

Mmoja wa wasanii watakao tumbuiza katika shindano la Redd's Miss Tanzania 2014, Ommy Dimpoz akipiga picha ya 'Selfie' na warembo wanao wania taji hilo Dar es Salaam leo wakati wa mkutano maalum na waandishi wa habari. Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee ndio watakao pamba shindano hilo linatakalo fanyika Oktoba 11, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.
Jumla ya warembo 30 watapanda katika jukwaa hilo kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa. Hadi sasa tayari warembo wa tano walioshinda mataji ya Miss Tanzania Photogenic 2014, Miss Tanzania Top Model 2014, Miss Tanzania Talent 2014, Miss Tanzania Sport Woman 2014 na Miss Tanzania Personality 2014 wamesha ingia nusu fainali za mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment