DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, October 31, 2014

PROF. JK MGENI RASMI UJENZI WA KITUO CHA MICHEZO KIDONGO CHEKUNDU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha michezo katika eneo la Kidongo Chekundi jijini Dar es salaam.
Kituo cha michezo kinajengwa kwa ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion Power na Serikali ya Tanzania.
Shehere hizo zinatarajiwa kesho asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.
Kwa mijbu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Symbion nchini Julie Foster , sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi. Margaret Byrne na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks
Taarifa hiyo imeongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa ujenzi huo Rais Kikwete atapanda mti kwenye eneo hilo, akisaidiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC Bi. Byrne, Mkurugenzi wa Biasharawa klabu hiyo Gary Hutchinson, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Hinks.

Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Barclays, Sunderland AFC inatoa usaidizi wa kiufundi na utendaji katika uendelezaji wa mradi wa mpira wa miguu, ambao ni wa kwanza na wa aina yake nchini humu, utakaohakikisha maelfu ya vijana wananufaika kutokana na mtazamo wa pamoja wa kuchanganya mpira wa miguu, elimu na ushiriki wa jamii, ili kupata ujuzi na utaalam wa Sunderland AFC.

No comments:

Post a Comment