Wanafunzi
ambao ni washindi wa shindano la kuandika barua wakiwa katika picha ya
pamoja na zawadi zao walizokabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu kwa niaba
ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa katika hafla ya
ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani 2014 yaliyofanyika
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dar es Salaam jana. Kutoka
kushoto ni mshindi wa kwanza kitaifa wa shindano hilo, Glory Mduma
kutoka Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi
wa pili, Ndehovye Nyindo wa Shule ya Lufingiro mkoani humo, na Mshindi
wa tatu, Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde
Juu. |
No comments:
Post a Comment