YAKIWA yamebaki majuma mawili kabla ya mahasimu wa jadi katika soka la
Tanzania kukutana klabu ya Simba inaondoka leo (Oktoba 8, 2014) kuelekea Afrika Kusini kupiga
kambi ya juma moja na nusu kujianda na pambano hilo lililopangwa kufanyika
Oktoba 18 uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati Simba ikienda Afrika
Kusini wapinzani wao Yanga bado hawaja weka wazi sehemu gani watakapokwenda
kupiga kambi kujiandaa na pambano hilo lenye upinzani mkubwa kwa soka la
Tanzania. Makamu wa Rais wa Simba Godrey
Nyange Kaburu, amesema timu hiyo itaondoka na wachezaji wake wote akiwemo kipa
Ivo Mapunda na watafanya mazoezi magumu ili kuweza kushinda mechi hiyo ambayo
ina umuhimu mkubwa licha ya kuwa na matokeo mabaya katika mechi zilizo pita.
“Kila kitu kimekwenda sawa
ikiwemo kuandaa Paspoti na viza za kuingilia Afrika Kusini matumaini yetu kambi
ya Afrika Kusini itakuwa ya mafanikio na kupata ushindi kama tulivyo
dhamiria,”amesema Kaburu. Simba imekuwa na mwenendo
mbaya tangu kuanza kwa ligi ya msimu huu na ina pointi tatu katika mechi tatu
ilizocheza ikiwa nyumbani uwanja wa taifa ambazo zote imeambulia sare.
|
No comments:
Post a Comment