Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Ben alihamishiwa katika hospitali hiyo akitokea Hospitali ya Jeshi ya Milambo mkoani Tabora alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya figo takriban majuma mawili yaliyopita. Ben Kiko atakumbuka kwa umahiri wake mkubwa katika tasnia ya habari hasa wakati akiripoti Vita vya Kagera mwishoni mwa miaka ya sabini moja kwa moja kutoka uwanja wa vita. (Vita ya Kagera ilihusisha nchi za Tanzania na Uganda ambapo Tanzania ilishinda vita hiyo).
Pumzika kwa amani somo wangu (BEN) wewe ni alama muhimu kwa taifa letu katika tasnia ya habari!
"MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI" | | |
|
No comments:
Post a Comment