DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, October 10, 2014

UHURU KENYATA NDIYO HABARI YA MJINI



PICHANI ni mapokezi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyerejea nchini kwake (Kenya) jana  baada ya kuhudhuria Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague nchini Uholanzi. Kenyatta alikanusha mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu wapatao 1,200 na wengine 600,000 kupoteza makazi. Kenyatta anakuwa rais wa kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC. Aidha, akihutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumpokea, Kenyatta alihimiza umoja, mshikamano, kusameheana na kuyatatua matatizo ya nchi hiyo kwa pamoja. 

No comments:

Post a Comment