DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, October 15, 2014

KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU CHAFANYIKA MKOANI TABORA JANA

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014, Rachel Kassanda akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete wa maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge huo kwenye uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora jana. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014 wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge huo kwenye uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora jana. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu  Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, 2014 kwenye uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora jana.

No comments:

Post a Comment