DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 08, 2016

HENRY AHOJI UWEZO WA ARSENAL MBIO ZA UBINGWA

Mchezaji nguli wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, mfaransa Thierry Henry ameuliza uwezo ‘mentality’ wa Arsenal katika harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini England,  baada ya kuukosa kwa zaidi ya miaka kumi hivi sasa.
Baada ya klabu ya Arsenal jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 nyumbani kwa Bournemouth mabao ya Oxlade Chamberlain na Mesut Ozil, kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger amejinasibu kuwa Arsenal bado wako katika mbio za ubingwa msimu huu, huku akiwataja Leicester kuwa wako katika nafasi nzuri zaidi katika mbio hizo.
Leicester City wamewafunga Liverpool na Manchester City ndani ya wiki moja na sasa wamekaa kileleni kwa tofauti ya points tano wakizipita Tottenham Hotspur, Arsenal na Manchester City.
Lakini Thierry Henry anasema klabu yake hiyo ya zamani haina mentality nzuri katika mbio hizo, huku akikumbushia mechi dhidi ya Chelsea na kudai kuwa ni mechi unahitaji kupata matokeo kama kweli unataka ubingwa.  Thierry pia amesema kuwa Leicester sasa wanaonekana kukomaa zaidi na anaamini lolote linaweza kutokea huku akiamini Leicester wana nafasi kubwa ya kuutwaa ubingwa huo wa England.
Kocha wa Leicester mara kadhaa msimu huu, amekua akiondoa imani hiyo kuwa timu yake iko katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa huo huku akisema kuwa wao hivi sasa wanaangalia zaidi mechi iliyopo mbele yao zaidi ya kuutizama msimu wote.

YANGA YAICHARAZA JKT RUVU 4-0

Ligi Kuu soka Tanzania Bara mzunguko wa pili umeendelea Jumamosi ya Februari 7, 2016 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, klabu ya JKT Ruvu ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Yanga katika mchezo wa marudiano, Yanga wamerejea katika furaha ya ushindi, baada ya kufanikiwa kuiadhibu JKT Ruvu kwa jumla ya magoli 4-0, licha ya kuwa walikuwa na wakati mgumu kuikabili Prisons ya Mbeya ktika mchezo wake uliopita baada ya kuambulia sare ya goli 2-2.

ALIKIBA AJA NA ‘LUPELA’

Ni siku mbili zimepita toka Alikiba alipoifanya pati ya kuitambulisha video yake mpya kwa Watanzania wachache waliopewa kadi za mwaliko, ila sasa hivi ameiachia video kwenye Youtube ili kila mtu aitazame… ni video ambayo aliifanya Marekani wiki kadhaa zilizopita…. ukishaitazama acha na comment yako hapo chini ili Alikiba akipita badae ajue mashabiki zake wanasemaje.

YASOMEKAVYO MAGAZETI JUMATATU YA FEBRUARI 08, 2016



































CONGO DRC YAKWAA UBINGWA WA CHAN

Timu ya taifa ya Jamuhuri ya kidemocras ya Congo imetwaa ubingwa wa kombe la Chan baada ya kuichapa Mali kwa mabao 3-0.
Magoli ya ushindi yalifungwa mchezaji Mechak Elia aliyefunga mara mbili,huku mshambuliaji Jonathan Bolingi akifunga bao moja
Na huu ni ubingwa wa pili kwa timu ya taifa ya Congo Drc chini ya mwalimu Florent Ibenge kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani .
Nayo timu ya taifa Ivory Coast imemaliza katika nafasi yaa tatu katika michuano hiyo baada ya kuichapa Guinea kwa Mabao 2-1.

TONI KROOS NI MCHEZAJI WA 3 KUVUTA MKWANJA MREFU REAL MADRID

Taarifa zimevuja juu ya mshahara anaokunja kiungo wa Real Madrid Toni Kroos lakini yeye akiwa ni mchezaji wa tatu kuvuta kitita kirefu cha fedha ndani ya Real Madrid akitanguliwa na mastaa wengine wawili.
Inakadiriwa kwamba mjerumani huyo anachukua kiasi cha dola 10.9m kwa mwaka lakini mashabiki wamekuwa wakihoji kuhusu kiwango anachokionesha ndani ya msimu huu.
Hakuna taarifa za uhakika zenye kuthibitisha ni wachezaji gani wawili ambao ndiyo wanavuta kitatita cha maana kwenye klabu hiyo, lakini wanadhaniwa kuwa ni Christiano Ronaldo na Gareth Bale au Sergio Ramos.
Madrid ililipa kiasi cha euro milioni 30 kwa ajili ya Kroos mwaka 2014 baada ya mcheaji huyo kuisaidia timu yake ya taifa ya Ujerumani kunyakua ndoo ya dunia. CHANZO: shaffihdauda.co.tz

WAZIRI MKUU MAJALIWA: NITAITISHA KIKAO CHA VIONGOZI WA DINI ZOTE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT,  Dkt.  Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu  huyo iliyofanyika kwenye Kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.

*******
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi karibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.
Ametoa ahadi hiyo jana mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alisema: “Hivi karibuni nitaitisha kikao cha viongozi wa dini zote kitakacho jumuisha Maaskofu Wakuu, Masheikh na baadhi ya wachungaji ili tukae na kubaini ni nini kifanyike ili kuisadia Serikali namna nzuri ya kuboresha maisha ya Watanzania.”
Akijibu risala iliyosomwa na Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dkt. Leonard Mwizarubi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kufanya mapitio ambayo yatawawezesha Watanzania kupata huduma kwa urahisi.
“Katibu Mkuu pamoja na Baba Askofu Mkuu wamegusia suala la upandaji wa gharama za vifaa vya ujenzi pamoja na suala la makazi bora. Mwezi ujao tunaanza vikao vya Bunge vya kupitia bajeti ya Serikali, tutaliangalia hili kwa kumshirikisha Waziri wa Fedha… tutafanya mapitio katika hili ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha,” alisema huku akishangiliwa na waumini hao.
Aliwaomba viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini wake waendelee kuiombea nchi pamoja na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwani kazi ya kutumbua majipu waliyoianzisha ina mitihani mikubwa.
“Kutokana na maombi yenu kwa viongozi wakuu wa kitaifa nina imani Taifa hili litafika tunakotaka liende. Endeleeni kutuombea kwa sababu kazi ya kutumbua majipu ina mitihani mikubwa. Lakini pia napenda niwahakikishie kuwa Serikali hii itatumbua majipu hayo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Hakuna mtu ambaye ataonewa,” alisisitiza Waziri Mkuu.
Kuhusu mgogoro wa kiwanja cha kanisa hilo kilichopo eneo la Ipagala, Waziri Mkuu aliahidi kulishughulikia suala lao kesho asubuhi kabla hajaondoka kurejea Dar es Salaam. “Kesho asubuhi nitamuita Mkurugenzi Mkuu wa CDA na kumtaka anipe taarifa sahihi kuhusu mgogoro huu. Najua suala hili liko mahakamani, lakini naamini Mkurugenzi anaweza kuwa kiungo kizuri kati ya wananchi waliojenga eneo hili pamoja na kanisa ambao mnamiliki kiwanja husika”.
“Kama atapata eneo jingine na kupima viwanja, kisha akawapatia hawa wananchi anaweza kuwa amesaidia kuondoa mgogoro huu. Wananchi walienda mahakamani huku wakijua eneo lenu limewekewa uzio, sasa wanagoma kutoka kwa sababu hawana mahali pa kwenda,” aliongeza.
Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Mwakipesile alisema kanisa litaendelea kuiombea Serikali ya awamu ya tano ili nchi idumu katika amani na utulivu.
Aligusia eneo la kanisa lililopo kiwanja na 34, kitalu ‘E’, Ipagala East, Dodoma, ambalo ujenzi wa shule yake umesimama kutokana na mgogoro baina yao na wananchi waliovamia eneo lao kwa kujenga nyumba za kuishi licha ya kuwa eneo hilo lilikwishawekewa uzio.
“Kama kanisa tumeshindwa kukamilisha ujenzi wa shule kwa sababu wananchi hao walifungua kesi mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Tunaomba uamuzi wa kesi hii uharakishwe,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema kanisa hilo lina majengo 4,670 nchini kote na viwanja 420 ambavyo ni vya kujenga makanisa na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mwizarubi alisema katika risala yake kwamba wanaiomba Serikali ifikirie kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kuwa na nyumba bora za kuishi.
“Maisha bora maana yake ni kuwa na nyumba bora. Tunaiomba Serikali yako ipunguze bei ya vifaa vya ujenzi ili Watanzania waweze kuwa na makazi bora,” alisema huku akishangiliwa.

JOSE MOURINHO KAVUNJA UKIMYA


Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, Februari 7, 2016 amerudi kwenye vyombo vya habari na kauli mpya baada ya kutokuwa tayari kuzungumzia soka. Jose Mourinho ameamua kuzungumzia soka ikiwa ni wiki sita zimepita toka afukuzwe kazi na Chelsea.
Jose Mourinho ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Man United ili arithi nafasi ya Louis van Gaal alikuwa hayupo tayari kuzungumzia soka, ila kwa sasa amekubali kulizungumzia suala hilo na kukiri kuwa hivi karibuni atarudi kazini, licha ya kuwa wengine huwa wanamtafsiri kama jeuri, lakini yeye anasema ni mtu wa kawaida na anajifunza popote.
“Siku zote nimekuwa nikijifunza hata katika sehemu ambayo najihisi ni mtaalam, siku zote mimi sio mkamilifu na nimekuwa nikijifunza kila siku, wakati mwingine katika kazi na hata maisha binafsi, narudi karibuni katika soka sehemu ambayo nahisi ni maisha yangu ya asili”  Alisema Jose Mourinho jana.

JK AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CCM CHAMWINO IKULU, DODOMA

Mjumba wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli akimkaribisha, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili, Ikulu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, kuendesha Kikao Maalum Cha Kamati Kuu  ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa na Mjumba wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli alipowasili, Ikuu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, kuendesha Kikao Maalum cha Kamati Kuu  ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM Februari 07, 2016 Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Rais Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM Februari 07, 2016 Chamwino mkoani Dodoma.
Add caption

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM Februari, 07, 2016 Chamwino mkoani Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu mwenzake, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Maaliwa.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM Februari 07, 2016 Chamwino mkoani Dodoma
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli kabla ya kikao kuanza. Katikati yao ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
 Viongozi hao wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale kabla ya kikao kuanza.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma Februari 07, 2016 kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Pombe Magufuli na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wajumbe wakisimama ukumbini kumlaki Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kabla ya kikao kuanza.
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk John Magufuli na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana na Asha Aboud wakibadilishana mawazo ukumbini.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Katibu wa NEC anayeshughulikia mambo ya Nje Dk. Asha-Rose Migiro ukumbini. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumkaribisha Mwenyekiti kufungua kikao.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu Maalum ya CCM, jana Februari 07, 2016 Ikulu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.