Taarifa zimevuja juu ya mshahara anaokunja kiungo wa Real Madrid Toni
Kroos lakini yeye akiwa ni mchezaji wa tatu kuvuta kitita kirefu cha fedha ndani ya Real Madrid akitanguliwa na mastaa wengine wawili.
Inakadiriwa kwamba mjerumani huyo anachukua kiasi cha dola 10.9m kwa
mwaka lakini mashabiki wamekuwa wakihoji kuhusu kiwango anachokionesha
ndani ya msimu huu.
Hakuna taarifa za uhakika zenye kuthibitisha ni wachezaji gani wawili
ambao ndiyo wanavuta kitatita cha maana kwenye klabu hiyo, lakini
wanadhaniwa kuwa ni Christiano Ronaldo na Gareth Bale au Sergio Ramos.
Madrid ililipa kiasi cha euro milioni 30 kwa ajili ya Kroos mwaka
2014 baada ya mcheaji huyo kuisaidia timu yake ya taifa ya Ujerumani
kunyakua ndoo ya dunia. CHANZO: shaffihdauda.co.tz |
No comments:
Post a Comment