DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 08, 2016

CHELSEA Vs MAN UNITED ZATOKA SARE YA 1-1

Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena jana Februari 7, 2016 kwa michezo miwili kupigwa, AFC Bournemouth walikuwa wenyeji wa Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani, wakati Chelsea  walikuwa wenyeji wa Man United katika dimba lao la Stamford Bridge, mchezo ambao ndio uliteka hisia za mashabiki wengi wa Ligi Kuu Uingereza.
Chelsea ambao bado wapo katika kipindi cha mpito chini ya kocha wao wa muda Guus Hiddink, wamefanikiwa kutoa sare ya goli 1-1, baada ya Man United kufunga goli la uongozi dakika ya 61 kupitia kwa  Jesse Lingard, wakati Man United wakiwa na matumaini ya kuondoka na pointi tatu, Chelsea walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 90 kupitia kwa Diego Costa na kufanikiwa kumaliza mchezo kuambulia kugawana pointi moja moja.
Kwa matokeo hayo Man United wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 41 katika michezo yao 25 waliocheza ya Ligi Kuu Uingereza hadi sasa, wakati Chelsea wapo nafasi ya 13 na pointi 30 wakiwa wamecheza michezo 25.

No comments:

Post a Comment