Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi amempongeza
Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kukubali uteuzi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) na GAVI utakaomfanya kuwa bingwa wa
chanjo na balozi wa mradi wa Africa United Duniani.
“Familia
ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika maendeleo ya
vipaji na wanamichezo kwa ujumla na jinisi chanjo inavyoweza kuwapa
watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali pia haki ya kuishi” ilisema
sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Katika
barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi wa Tanzania
akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha sasa na kijacho
katika Afrika na dunia kwa ujumla.
“TFF
itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na
ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa
kwa Rais wa Caf, Issa Hayatou. |
No comments:
Post a Comment