Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, Februari 7, 2016 amerudi kwenye vyombo vya habari na kauli mpya baada ya kutokuwa tayari kuzungumzia soka. Jose Mourinho ameamua kuzungumzia soka ikiwa ni wiki sita zimepita toka afukuzwe kazi na Chelsea.
Jose Mourinho ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Man United ili arithi nafasi ya Louis van Gaal alikuwa
hayupo tayari kuzungumzia soka, ila kwa sasa amekubali kulizungumzia
suala hilo na kukiri kuwa hivi karibuni atarudi kazini, licha ya
kuwa wengine huwa wanamtafsiri kama jeuri, lakini yeye anasema ni mtu wa
kawaida na anajifunza popote.
|
No comments:
Post a Comment