Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametangaza baa la njaa linalokabili taifa hilo la kusini mwa Afrika kuwa janga la kitaifa.
Taifa
hilo halijapokea mvua ya kutosha tangu mwaka jana na watu 1.5 milioni
wanahitaji msaada wa chakula, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Maelfu ya mifugo wamefariki kutokana na ukame.
Tangazo
hilo la Rais Mugabe limejiri siku chache tu baada ya Muungano wa Ulaya
(EU) kumhimiza atangaze baa hilo kuwa janga la kitaifa ili mashirika ya
kimataifa ya misaada yaweze kuchangisha pesa haraka za kusaidia raia wa
Zimbabwe. |
No comments:
Post a Comment