DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 08, 2016

VAN GAAL AKANUSHA UVUMI KUHUSU JOSE MOURINHO

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amekanusha uvumi kuwa aliyekuwa meneja wa Chelsea Jose Mourinho kurithi kiti chake Old Traffod hivi karibuni.
Mourinho, aliachishwa kazi kutoka Chelsea mwezi Desemba, mwaka jana (2015).
Mourinho, aliwaahidi mashabiki wake kuwa atarejea karibuni na kudokeza kuwa wakala wake alikuwa amefanya mazungumzo na Manchester United.
Van Gaal alisema
"kwa kweli kuna mambo mengi tu ya porojo ambayo yameandikwa kunihusu mimi.
''Ukweli hata sasa siamani kuwa kuna uhusiano wa aina yeyote kati ya aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho na Man United huo ni Uvumi!."

Mourinho kwa upande wake alinukuliwa akiwaambia waandishi wa habari kuwa ''mimi ninapenda ushindani kila siku.

''kwa hakika nitarejea hivi karibuni uwanjani'' Mreno huyo aliiambia jarida la Mail on Sunday.
Timu ya Manchester United imekataa kusema lolote juu ya madai kuwa ilifanya mashauriano na wawakilishi wa kocha Mourinho.
Habari za kuaminika hata hivyo zinasema kuwa mashauriano yamefanywa na Mourinho - ambaye ametajwa kama mmoja wapo wa makocha wanaowania kazi katika timu ya Manchester United ambayo imetapatapa kwa muda na ambayo kocha wake wa sasa, Lous Van Gaal, anatarajiwa kuondoka baadaye mwakani.
Japo uvumi huo unaendelea kuenea, Van Gaal angali anakipindi cha mwaka mmoja zaidi katika kandarasi yake na United.
Mourinho, amewahi kuhudumu Inter Milan na Real Madrid baada ya kuondoka Chelsea 2007.
Hata hivyo mwaka huu amesisitiza kuwa familia yake itasalia nchini Uingereza.
Katika kipindi cha wiki mbili kazi ya Van Gaal imekuwa ikiyumba yumba.
Hata hivyo, ushindi dhidi ya Stoke na Southampton kumesababisha kuimarika kwa timu hiyo.
United ambao wana alama tano nyuma ya Arsenal inayoshikilia nafasi ya nne kwa alama 45.


No comments:

Post a Comment