Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa Dkt.
Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika
(kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa
usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kufuatia
uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi
za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma
makao makuu ya AU na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu
alilokabidhiwa.
Mheshimiwa
Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani
kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.
Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
Naye
Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na kuwa
tayari kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika
nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake.
Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha
katika kutekeleza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment