DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, February 02, 2016

SAMATTA ATUA RASMI KRC GENK, ACHAGUA JEZI KUVAA NAMBA 77

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta Januari 29, 2016 taarifa za yeye kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji zilianza kuenea, na baadae kuthibitika baada ya picha za utambulisho wa staa huyo kuanza kuenea mitandaoni. Mbwana Samatta ambaye amekabidhiwa jezi namba 77.  
“Nimechagua jezi namba 77 kwa sababu wachezaji niliokuwa nawapenda mimi kama akina Eric Cantona, Cristiano Ronaldo na David Beckham walikuwa wanavaaa jezi namba 7, Mr Dimitri alivyoniuliza napenda kuvaa jezi namba ngapi nilimwambia jezi 77 kwa maana sikutaka kugombania namba ya jezi, kwa kila klabu unayokwenda ni ngumu kukuta jezi namba 7 haina mtu, sasa sikutaka kugombania namba ya jezi lakini mimi pia ni shabiki wa Man United” alisema Samatta.

No comments:

Post a Comment