DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, January 29, 2015

JANUARY MAKAMBA NA ARI YA KUINUA VITUO VYA MICHEZO VYA KANDA

Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi karibuni pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa January Makamba(Pichani juu)  hivi karibuni ameainisha adhma yake ya kuinua kiwango cha michezo nchini.
Azma hizo zimo katika  katika mazungumzo yake na Padre Privatus Karugendo ambayo yamechapishwa katika kitabu ambacho gazeti hili imekipata nakala yake ambapo ameainisha azma ya kujenga vitua vya michezo vya kanda vyenye hadhi ya kiolimpiki.
Kwenye kitabu hicho, Makamba amejibu swali kwamba kitu gani kifanyike ili Watanzania waweze kujivunia wanamichezo wao. Makamba alisema, “Inafedhehesha sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho tumeshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika.
Mwaka huo huo wa 1980 ndio mara ya kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda medali za Olimpiki. Rafiki yangu Mzee Suleiman Nyambui na Mzee wetu Filbert Bayi ndio walitutoa kimasomaso kipindi kile. Ni muhimu kurekebisha hili.” 
Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu katika medani ya kimataifa huku tasnia ya michezo ikiendelea kugubikwa na migogoro isiyokwisha. Kutokana na migogoro hii, Tanzania inaendelea kupoteza matumaini ya kung’aa katika medani za kimataifa. 
Katika mazungumzo hayo na Padre Karugendo, Makamba  alinukuliwa akisema, “Lazima tutambue kwamba maendeleo ya michezo yanatokana na vitu muhimu vitatu. Kwanza, ni lazima kuwepo na vipaji, bahati nzuri nchi yetu ina vipaji vya kutosha katika aina zote za michezo. Pili, ni miundombinu na mfumo wa kubaini na kuviendeleza vipaji hivyo, hii  bado ni changamoto . Tatu, ni utawala, uongozi, na uendeshaji wa tasnia ya michezo, hii pia ni changamoto. Hivi vitu vitatu ni lazima viwepo ili tuweze kupata mafanikio kwenye medani ya michezo.”
Kama mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makamba anaungwa mkono na vijana wengi kutokana na kuendesha siasa zake kisasa, kibunifu na kuepuka malumbano ya jukwaani.
Katika mazungumzo hayo Makamba alielezea fikra zake alizonazo hasa hasa kwenye kuendeleza vipaji vya Watanzania ambapo alisema, “Ni lazima tuanzishe vituo vikubwa vya michezo au ‘sports academies’ kwenye kila kanda ya nchi yetu vyenye hadhi ya Kiolimpiki.” 
Makamba aliongeza  kwamba, “Kutakuwa na vituo sita vya aina hii katika nchi yetu ambavyo vitazungukwa na shule za msingi na sekondari za ‘boarding’. Vituo hivi vitakuwa na lengo la kukusanya wanafunzi wote kwenye kanda husika ambao wameonekana kuonyesha vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa. Ukweli ni kwamba bila kuendeleza vipaji katika mazingira mazuri, basi tusahau kabisa kufanya vizuri kwenye michezo. Hili linaweza kufanywa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi”.
Mheshimiwa January Makamba anakuwa mgombea wa kwanza wa Urais kuweka bayana mipango yake ya Tanzania Mpya katika maandishi. Anaendelea kufunguka kwamba katika tasnia ya michezo ni muhimu sana kuwekeza katika watoto. Zaidi ya hapo, kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na akademi na TFF iendeshe ligi kuu ya timu za watoto.
“Tufikie wakati ambapo timu za taifa za miaka 10 ijayo ziwe zinaandaliwa kuanzia sasa, na serikali itenge bajeti kila mwaka kwa timu hizo  ili kuziwezesha kukaa kambini, kufanya mechi za majaribio na kuziwezesha kushiriki kikamilifu katika mashindano ya kimataifa. Mimi sio muumini wa hizi kamati za zimamoto kusaidia timu ishinde ghafla ghafla wakati siku zote watu hawafanyi maandalizi ya muda mrefu” alimalizia Makamba.
Makamba pia aligusia kuhusu suala la ukata na ufinyu wa bajeti unaokabili tasnia za michezo. Siku zote tunaona timu za taifa za olimpiki au jumuiya ya madola kukosa fedha za kukaa kambini ambapo huchangia katika matokeo hafifu.
“Huko nyuma, taasisi na mashirika ya umma yalikuwa na timu za michezo zilizokuwa zinafanya vizuri na kutoa michango kwenye maendeleo ya michezo. Kwa mfano, Pamba ya Mwanza, Sigara, Reli ya Morogoro, ushiriki huu ulichangamsha sana michezo na ni lazima turudishe utamaduni huu,” alimalizia Makamba.
 
 

Wednesday, January 28, 2015

NSSF, REALREAL MADRID ZAPANIA KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau  akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya shirika hilo na timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk. Dau alisema katika uendeshaji wa kituo hicho, Real Madrid itakua na dhamana ya kushughulikia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (kulia) wakibadilishana mikataba ya kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya timu yake  na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kitahusisha wanafunzi 108 watakaogawanywa kwenye timu za chini ya umri wa miaka 13, 15, 17, 19, kikosi cha pili na timu ya wakubwa.

WAZIRI MAGUFULI AZINDUA MIRADI SITA YA UJENZI WA BARABARA ZA KUPUNGUZA MSONGAMANO KATIKA JIJI LA DAR

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba- Tangi Bovu.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya External –Kilungule.
Uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Kigogo-Tabata dampo.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Msewe-Baruti.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kushoto akiwa na mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida kulia wakifurahia mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba –Tangi bovu.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akisalimiana na wananchi kabla ya uzinduzi wa miradi hiyo ya kupunguza msongamano.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiwashika mikono Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mheshimiwa John Mnyika pamoja na mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee mara baada ya kuzindua mitambo itakayofanya kazi katika ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba –Tangi bovu.
Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa John Mnyika akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi katika shule ya Msingi Msewe.
Taaswira ya barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangi bovu eneo la Goba ambalo limeshajengwa kwa kiwango cha lami. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi).

MHE. UMMY MWALIMU AKABIDHIWA OFISI RASMI NA KAIRUKI

Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu wakati akimkabidhi ofisi jijini Dar Es Salaam kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililofanyika Januari 24, 2015.

SIMBACHAWENE AANZA KAZI RASMI WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye eneo la kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuchakata gesi cha Kinyerezi.
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima ( aliyetangulia mbele) akiongoza msafara wa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene kwenye eneo la mradi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Sehemu ya mtambo wa kuchakata gesi wa Kinyerezi.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage.
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (katikati) akielezea maendeleo ya mradi wa Kinyerezi I. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene. Kushoto kabisa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio (kushoto) akimueleza Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (wapili kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava na Naibu Waziri wa Wizara hiyo anaeshughulikia Nishati, Charles Mwijage (kulia) juu ya hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji wa kituo cha kuchakata gesi cha Kinyerezi I pamoja na ujenzi wa bomba la   gesi kutoka Mtwara hadi  jijini  Dar es Salaam walipotembelea kituo hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene na  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (katikati)  wakiwa katika picha ya  pamoja na watendaji wa Wizara  ya Nishati na Madini na wataalamu wa mradi wa kuchakata gesi wa Kinyerezi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi.
Mtaalamu kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro iliyopewa kazi ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I Clas-Eirik Strand (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) Katikati ni Meneja Mradi wa Kinyerezi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima.

YALIYOJILI BUNGENI JANA

 Spika wa Bunge, Anne Makinda akiongozwa na Mpambe  kuingia kwenye ukumbi wa Bunge  Januari 27, 2015.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiapa Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akimpongeza Mwanasheria Mkuu wa serikali, George  Masaju (wapili kulia) baada ya mwanasheria huyo kuapishwa Bugeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama,Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua nasari, Bungeni Mjini Dodoma Januri 27, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Momose Cheyo, Bungeni mjini Dodoma Januri 27, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Juliet Masaju (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum, Felista Bura (katikati) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Januari 27, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na mbunge wa igalu, Mhandisi Athumani Mfutakamba (kushoto) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Januari 27, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma  Januari 27, 2015.

Tuesday, January 27, 2015

KINANA NDANI YA JIMBO LA MTAMBWE, PEMBA

Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa halmashauri Kuu ya Wilaya ya Wete, ambapo alisomewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mkoa wa Kaskazini Pemba na wilaya hiyo.
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana ukielekea Jimbo la Mtambwe kwa kutumia barabara ya kisasa iliyojengwa na Selikali katika Jimbo hilo alilozaliwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad. Katika jimbo hilo Kinana alizindua pia mradi wa utandazaji wa bomba lamji na usimikaji wa nguzo za umeme.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiweka kifaa cha umeme kwenye transfoma wakati wa uzinduzi wa uwekaji nguzo za umeme katika Kijiji cha Chanjaani, Jimbo la Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Zanzibar leo. Jimbo hilo ndilo alikozaliwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Jengo la Ofisi za CCM Tawi la Bopwe, mjini Wete.
Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinaa akishiriki kupaka rangi majiko ya Mseredani (majiko ya mkaa yanayotengenezwa kwa udongo) katika kikundi cha vijana Jimbo la Gando, wilayani Wete.
Kinana akipata maelezo kuhusu zao la karafuu alipokwenda  kuona ununuzi wa Karafuu katika Ghala la Serikali la ZSTC, wilayani Wete leo.Kushoto ni Mkulima wa zao hilo na Issa Hassan ambaye ni Meneja Utawala wa ZSTC.
Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM wakifukia mabomba ya maji safi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Jimbo la Mtambwe, wilayani Wete.
 Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Maskani ya Chekea  iliyopewa jina na Dk, Jakaya Kikwete katika Jimbo la Mtambwe ambapo vijana wa CUF 35 wamehamia CCM. Vijana hao walidai wameamua kuhamia CCM baada ya kuchoshwa na ahadi hewa za viongozi zikiwemo za Maalim Seif Sharrif Hamad. Pia wameahidi kuwashawishi vijana wengine wa CUF kujiunga na CCM.
Vijana wa Mtamwe wakishangilia baada ya Mbunge wa CCM Viti Maalumu, kuwaahidi mbele ya Kinana kuwa atawapatia jezi seti mbili kwa ajili ya mchezo wa soka.
Kinana akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi walipowasili kwenye Chuo cha Ualimu cha Benjamini Mkapa kuzungumza na Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Uoja wa Vijana wa CCM, Shaka, akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.
 Wafuasi wa CCM wakicheza kwa furaha katika mkutano huo.
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo.
 Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano huo uliofanyika eneo la Mtemani, Mjini Wete.