Timu
za soka za Simba na Azam leo zimetoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa
ligu kluu soka Tanzania uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao hayo yalifungwa na Emmanuel Okwi upande wa Simba na Kipre Cheche
upande wa Azam.
Aidha
katika mchezo huo Mshambuliaji mganda wa Simba, Emmanuel Okwi
aligongana na Agrey Moris na klupoteza fahamu jambo ambalo lilipelekea
kutolewa nje ya uwanja kwa machela na vbaade kupelekwa Muhimbili kwa
matibabu zaidi
Pichani
ni Okwi akiwa chini uwanjani huku daktrai wa Simba Yassin Gembe akitoa
huduma ya kwanza kabla ya mwamuzi kuomba atolewe nje kwa matibabu
zaidi.
Aidha
kwa mujibu wa daktari huyo wa Simba, Yassin Gembe, Okwi aligongwa
sehemu ya kichwa na kupelekea kupoteza fahamu na yupo Muhimbili kwa
matibabu zaidi na hali yake inaendelea vizuri na kuwatoa hofu mashabiki
na wapenzi wa Simba.
|
No comments:
Post a Comment