DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, January 27, 2015

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI UJERUMANIKWA ZIARA YA KIKAZI


Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia ya marehemu  mjini Riyadh, Saudi Arabia Januari 25, 2015 mara alipofika kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Januari 22, 2015 na kuzikwa Januari 23, 2015. Baaada ya tendo hilo Rais Kikwete aliendelea na safari kuelekea nchini Ujerumani na Ufaransa kwa ziara ya kikazi.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani jana kuungana na viongozi mbalimbali duniani  kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa kwa nchi zinazoendelea. (Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment