DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, January 21, 2015

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YAFURAHISHWA NA MIRADI YA VIJANA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda akizungumza na wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke kamati hiyo ilitofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika manispaa hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Maabad S. Hoja na wamwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo. 
Mwenyekiti wa Temeke Vijana Saccoss Bw. Swaka Abbas akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya Saccoss yao mbele ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilifanya ziara ya kutembelea niradi ya inayoendeshwa na Vijana kupitia Vikundi vilivyopata mkopo kutoka katika Mfuiko wa Maendeleo ya Vijana

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Maabad S. Hoja akifafanua jambo wakati wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyopata mkopo kutoka Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Bw. P. Kagimbo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia (MB) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda.
Baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo jana.
Kushoto ni mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Dkt. Maua Daftari akifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo.

No comments:

Post a Comment