MIAMBA
ya soka kutoka Magharibi mwa Afrika, Ivory Coast imeanza kwa sare ya
1-1 dhidi ya Guinea katika mechi ya kundi D , michuano ya mataifa ya
Afrika inayoendelea huko Guinea ya Ikweta.
Guinea
walikuwa wa kwanza kufunga goli katika dakika 36' kipindi cha kwanza
kupitia kwa nyota wake Mohamed Yattara, hata hivyo Ivory Coasta
walisawazisha dakika ya 72' kupitia kwa Seydou Doumbia.
Nayo mechi ya pili ya kundi kund hilo baina ya Mali na Cameroon imemalizika kwa sare ya 1-1.
Mali
waliandika bao la kuongoza dakika ya 71' kupitia kwa Yambou Yatabare,
lakini Simba wasiofugika, Cameroon wakasawazisha kupitia kwa Ambroise
Oyongo Bitolo.
Kufuatia kumalizika kwa mechi za kwanza za kundi D, michuano hiyo leo inaendelea kwa mzunguko wa pili wa makundi.
Timu za
kundi A zinaanza kutupa karata yao ya pili ambapo mechi ya kwanza
itawakutanisha wenyeji Guinea ya Ikweta dhidi ya Burkinafaso ambao
walipoteza mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 dhidi ya Gabon.
Mechi ya pili inayoanza majira ya saa 4:00 usiku leo, itawakutanisha Congo na Gabon. |
No comments:
Post a Comment