DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, January 21, 2015

WAZIRI WA MAJI PROF. JUMANNE MAGHEMBE AMETOA SIKU 90, KWA MKANDARASI MEGHA ENGINEERING

Waziri wa maji Jumanne Maghembe wa kwanza kulia akizungumza na wakandarasi wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati alipotembelea tembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji Taka (DAWASA),  kwalengo la kupata tathimini ya mradi huo ulipofikia sasa.
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe (wapili kulia) akioneshwa mchoro wa mradi wa bomba la maji  Mlandizi Kimara linalopitia Makongo Juu na Mhandisi wa Mradi huo, Bw. Severin Mkendala jinsi mabomba  mradi wa Mlandizi Kimara yalipopita.
Kushoto ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearing Infrastructure Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa katika ziara  ya kutembelea miradi  inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Mghembe (wapili kulia) akiwa ameongozana na meneja mradi Pintu Dutta (watatu kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa kituo cha kusafisha maji cha Ruvu juu.
Mtambo aina ya Catterpilar wa kampuni ya Megha Enginearing Infrastructure Limited, ukiwa unasafisha eneo ambalo linatakiwa kulazwa mabomba yanayotoka Mlandizi Kimara kwenda Ruvu Juu.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilisha ziara hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya WABAG Constraction wakiendela na ujenzi wa kituo cha kusafisha maji cha Ruvu Juu .

No comments:

Post a Comment