Mfalme Abdullah Bin Abdulaziz akiwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
*************
MFALME wa Saudi Arabuia, Abdullah bin
Abdulaziz amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 90.
Mfalme Abdullah aklikuwa amelazwa
hospitalini kwa matibabu ya maradhi yalikuwa yakimkabili tangu m,wezi Desemba
mwaka jana.
Kufuatia kifo chake Mdogo wake aitwaye, Salman,
79, amemrithi katika ufalme huo.
Kifo chake kilithibishwa jana katika
matangazo katika televisheni ya taifa ambapo ilikuwa ikitolewa mistari Quran ambayo hutolewa tu endapo kuna kifo cha
mtu mzito katika familia ya kifalme.
Mazishi ya Mfalm,e Abdullah yanataraji
kufanyika leo kwa kufuata tamaduni za kiislamu ambapo mtu hutakiwa kuzikwa
ndani ya saa 24 tangu kifo chake.
Viongozi mbalimbali Duniani akiwemo Rais
Barack Obama ametuma salamu za rambi rambi.
|
No comments:
Post a Comment