Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa
pili kulia) akiongoza na viongozi wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na maafisa wa Serikali
alipofanya ziara ya kushtukiza leo jijini Dar es salaam katika soko la
Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia
matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia
mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na
kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Wa kwanza kulia ni Kaimu
Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani,
wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala Elias Balongo
na kushoto mwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf
Mkenda. |
No comments:
Post a Comment