BAADA
ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya kulevya 'unga' na baadaye
'kustaafu', madawa hayohayo yamemletea msanii Rehema Chalamila 'Ray C'
'dhoruba' ambayo imemfanya yeye mwenyewe, kwa hiyari yake ajisalimishe
polisi.
KAWE DARAJANI Chanzo
hicho kilieleza kwamba, siku ya tukio, wakati Ray C akitokea
nyumbani kwake, alipofika maeneo ya Kawe Darajani aliona pikipiki
ikimfukuzia na baadaye ikampita na 'kumbloku'. Ilisemekana
kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka kwenye pikipiki kisha
akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya Toyota Carina TI.
Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi. "Ray
C aliamua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo
kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi," alisema.
LUGALO Ilisemekana
kwamba baada ya kufika kwenye kituo cha daladala cha Lugalo, alisimama
na jamaa huyo aliyekuwa akimfukuzia akaegesha pikipiki mbele yake na
kumtaka Ray C ashuke ndani ya gari kwani alitaka kulipekua akimwambia
kuwa alikuwa amebeba unga. Ishu hiyo ilizidi kumtia Ray C wasiwasi na kumuuliza jamaa huyo ni nani ambapo alisema kuwa yeye ni askari. Kwa kuwa hakuwa na sare, Ray C hakuamini jambo lililosababisha jamaa huyo kumuonesha kitambulisho kilichokuwa kimechakaa.
MAELEWANO YASHINDIKANA Baada
ya kuona hivyo, Ray C alimwambia waongozane hadi Kituo cha Polisi cha
Oysterbay lakini jamaa huyo alikataa na kumtaka waende Kawe jambo ambalo
Ray C alishindwa kuafikiana nalo na kuondoa gari lake akimwambia
waambatane hadi Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge.
Jamaa
huyo alionekana kutotaka kwenda hivyo Ray C aliondoa gari kwa kasi na
kuelekea Mwenge ambako alikuwa akiomba msaada kwa matrafiki na alipoona
wanachelewa aliondoa gari kumkimbia jamaa huyo. Ilisemekana
kwamba awali alitaka kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mwenge lakini
alipoona kuna msongamano alikimbia kwenda kujisalimisha Mabatini huku
akiangua kilio.
Baada ya kushibishwa taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ray C ambaye alielezea mkasa mzima. Alifunguka:
"Ni kweli ulivyoambiwa tulitoka Lugalo na kuelekea Mwenge baada ya
kufika kwenye makutano ya Mwenge niliwaona askari wawili na trafiki
akiwa pembeni, nikawasimamisha na kuwaeleza. "Askari mmoja alikubali kupanda kwenye gari langu nikaenda naye hadi Mabatini.
"Baada ya kufika Mabatini nilieleza kila kitu kwa mkuu wa kituo hivyo akaniambia nisiwe na wasiwasi. "Bada
ya hapo mkuu wa kituo aliita askari wa kike na wa kiume nikaongozana
nao hadi katika gari langu na kupekua kila sehemu lakini wakasema
hapakuwa na chochote kibovu, hivyo nikawa nalia tu na mkuu wa kituo
akaniomba ninyamaze na kuniruhusu nikaondoka zangu kwenda Hospitali ya
Mwananyamala kumeza dawa. (Chanzo: Global Publishers)
|
No comments:
Post a Comment