DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, January 02, 2015

DKT. BILALI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA PAMOJA NA KUIOMBEA TANZANIA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam juzi usiku Disemba 31, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la mkesha wa Mwaka Mpya (2015) na Dua maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania.
 Wananchi mbalimbali wa jijni Dar es salaam na mikoa jirani wakishangilia kwa furaha wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akihutubia Taifa kwenye Tamasha la Mkesha wa mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika Disemba 31, 2014 usiku wa kuamkia mwaka mpya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Taifa kwenye Tamasha hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Viongozi na Wananchi kupeperusha bendera ya Taifa mara baada ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 kwenye Tamasha la mkesha na Dua maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania, sherehe ambazo zilifanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam juzi usiku Disemba 31, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwatakia heri ya mwaka mpya wa 2015 Viongozi na Wananchi baada ya kumalizika kwa Tamasha na Dua maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  Disemba 31, 214.

No comments:

Post a Comment