Baadhi ya waandishi na maofisa
mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia maelezo ya
kujiuzulu Waziri Prof. Sospeter Muhongo hivi karibuni.
**********
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri.
Prof. Muhongo ametangaza uamuzi huo
asubuhi ya leo katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa
mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini.
Akitangaza uamuzi huo Prof. Muhongo
amesema ameamua kuachia wadhifa huo ili kupisha nchi ijadili na kufanya
mambo muhimu ya maendeleo badala ya kuendelea kujadili masuala ya
Escrow.
"Wananchi wamechoka, na hata mimi
mwenyewe nimechoka kila kukicha watu wanajadili ESCROW, hivyo anajiuzulu
ili watu wafanye kazi na kuleta maendeleo," alisema prof Muhongo.
Aidha amesema sakata yeye anaendelea
kusisitiza na kusimamia msimamo wake kuwa hahusiki kwa namna yeyote ile
katika uchukuaji wa fedha za akaunti ya Escrow kama inavyodaiwa na watu.
Waziri huyo amejiuzulu ikiwa ni baada
ya kuitumikia wizara hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tu, huku
akiwa amefanya jitahada kubwa kuhakikisha wananchi vijijini wanapatiwa
umeme kwa gharama nafuu.
Muhongo amesema ni wakati mzuri sasa
kuviachia vyombo vya dola hasa Mahakama kujadili suala la Escrow nasio
watu wengine mitaani.
|
No comments:
Post a Comment