DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, September 09, 2015

WENGER AMSHAURI HENRY

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye amewahi kumfundisha Thierry Henry kama mchezaji wake kwa miaka mingi, Wenger amemshauri Thierry Henry kama kweli ana nia ya dhati ya kutaka kupata mafanikio kama kocha katika soka.

Wenger amemshauri Henry ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Arsenal chini ya umri wa miaka 18 kuwa, kama kweli anataka kupata mafanikio katika ukocha inabidi apate ushauri wa kisaikolojia katika akili yake. Henry anafundisha kikosi hicho cha vijana huku akipata mafunzo  ya ukocha.

Henry ambaye anaheshima ya kuwa mfungaji bora wa klabu ya Arsenal kwa muda wote, alisajiliwa na Wenger akitokea klabu ya Juventus ya Italia mwaka 1999 ila Wenger amemueleza utofauti uliyopo kati ya kuwa mchezaji na kuwa kocha.

ABIRIA 159 WA NDEGE YA BRITISH AIRWAYS WANUSURIKA KIFO

Kama hii dharura ingetokea wakiwa katikati ya safari basi vyombo vya Habari Duniani vingekuwa na stori tofauti kabisa… Ndege ya Shirika la British Airways ilikuwa tayari kwa ajili ya safari kutoka Uwanja wa Ndege Las Vegas Marekani, ndani kulikuwa na abiria 159 pamoja na wahudumu wa Ndege 13.

Ajali hiyo ilitokea ghafla ambapo injini ya kushoto ilishika moto wakati ndege hiyo tayari ilikuwa kwenye njia ya kuruka… ikabidi safari iishie hapo na abiria wote watoke ndani ya Ndege kwa dharura.

Majeruhi ni wachache ambao walipata majeraha madogo madogo lakini hakuna taarifa ya mtu yoyote kufariki.

Muda mfupi baadae Rubani mmoja wa Ndege hiyo aliwaambia abiria hao kwamba ana uzoefu na kazi ya Urubani kwa muda mrefu lakini hakuwahi kupata tatizo la aina hiyo katika kazi yake, na chanzo cha moto huo ilikuwa ni tatizo la kiufundi kwenye injini ya Ndege hiyo.

Sunday, September 06, 2015

RANSEY NOUAH AKATAA SIASA

Muigizaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, Ramsey Nouah.

Muigizaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, Ramsey Nouah amekaririwa akisema kuwa, yuko tofauti kabisa na wasanii wenzake wa nchini humo wanaokimbilia kwenye siasa kila kukicha na kuongeza kuwa mashabiki wake wasitegemee Ramsey kujiunga na siasa.
Akifanyiwa mahojiano maalum na mtandao wa NET wa nchini humo, Ramsey alisema kuwa: ‘Sijui jinsi gani naweza kuwa mwanasiasa, mimi sio mwanadiplomasia kivile. Sijui namna ya kuyapangilia maneno yakafana kama wanasiasa wanavyoweza kufanya. Mimi siko hivyo’ Alisema Ramsey Nouah. Na NaijaGists.com

MAGUFULI: SIKO TAYARI KUTOA AHADI HEWA!


 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimwombea sala  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli  mara baada ya kumaliza kuhutubia  jioni ya jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni ya jana.
 Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli  ukikatiza kwenye dara la muda la Mto Kilombero, ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli  akikagua daraja la Mto kilombero ambalo ujenzi wake unaendelea mpaka sasa. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  akipata maelezo mafupi kuhusia na maendeleo ya ujenzi wa dara hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Kilombero,litapunguza kero kubwa ya usafiri miongoni mwao kwa kiasi kikibwa.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
Wanafuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM jioni ya leo mjini Ifakara

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Udiwani wa CCM wilaya ya Ulanga jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msinfi Mahenge jioni ya jana.
Mgombea ubunge jimbo la Kilombero Ndg. Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani akizungumza jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero jioni ya jana.

Wananchi wa mji wa Ifakara walaiojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo. 
Wananchi wa Kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero wakiwa wamefunga bara bara wakimsimamisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli  awasalimie alipokuwa akitokea Malinyi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Saba saba jioni ya jana.

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake atahakikisha baadhi ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa marais waliomtangulia,amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya wananchi ili awe Rais hatakuwa tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni dhambi na kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.
Akizungumza kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais, Dk.Magufuli aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi waliomtangulia kuongoza nchi.Alisema sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo marais ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na awamu ya nne.“Iwapo nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza .Yupo mzee Ali Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman Abeid Karume.“Huu ndio utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa ushauri katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania.Najua msimamo wangu na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu.Narudia tena kwangu mimi ni kazi tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili nifikie malengo yangu,”alisema.Alisema kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.

Dk.Magufuli ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara Mkoa wa Morogoro.

MATOKEO YA BAADHI YA MECHI ZA KUFUZU AFCON HAYA HAPA .

Djibouti 0-2 TogoNamibia 0-2 SenegalComoros 0-1 UgandaBurundi 2-0 NigerRwanda 0-1 GhanaTanzania 0-0 NigeriaSeychelles 1-1 Ethiopia

KAMPENI ZA URAIS: LOWASSA ATUA TABORA!

Aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja akiuhutubia Umati wa wakazi wa Mji wa Tabora, waliofutirika kwa wingi kwenye Uwanja wa Town School, kulikofantika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa, jana Septemba 5, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, akilakiwa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Tabora, wakati akipita kuelekea jumwaa kuu, wakati wa Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa, jana Septemba 5, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, akimwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, jana Septemba 5, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa, wakati alipowasini kwenye Uwanja wa Town School, kuhudhulia Mkutano wa Kampeni, jana Septemba 5, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye, akisisitiza jambo katika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, jana Septemba 5, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipanda jukwaani kwa kukimbia mara baada ya kutua na Chopa yake, jana Septemba 5, 2015.
Meza Kuu.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Tabora, jana Septemba 5, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia na kunadi sera zake kwa wananchi wa Mji wa Tabora, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika jana Septemba 5, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi wa Tabora.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wake, Mhe. Freeman Mbowe, wakati wakitoka kwenye Mkutano wa hadhara wa Kampeni, Mjini Tabora jana Septemba 5, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakicheza sambamba na wananchi wa Tabora, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Town School, mjini humo jana Septemba 5, 2015.



Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti kwa mgombea wao!

Thursday, September 03, 2015

ALIKO DANGOTE ATUA ZIMBABWE

Mwanaume tajiri  kuliko wote Afrika, Aliko Dangote anaziandika headlines zake kwenye kurasa za biashara na uwekezaji barani Afrika. Baada ya kuweka wazi mipango alionayo juu ya Tanzania time hii ameweka wazi mipango mingine alionayo juu ya nchi zingine za Afrika.
Safari hii ni zamu ya Zimbabwe kukamata fursa zinazoletwa na Dangote nchini kwao… Tajiri Dangote ameweka wazi mipango yake ya kuwekeza dola million 400 (Bilioni 800 za Tz) kwenye ujenzi wa kiwanda kikubwa cha simenti nchini humo.
Aliko Dangote na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Aliko Dangote aliweka wazi mipango hii siku ya Jumatatu akiwa kwenye press conference na waandishi wa habari jijini Harare baada ya kukutana na Rais waZimbabwe Robert Mugabe na Makamu wa Rais  Emmerson Mnangagwa.
“Tumeamua kuwekeza ndani ya Zimbabwe, ndio maana tupo hapa. Nchi yoyote utakayoona tunaitembelea inamaanisha, ndio, tumeamua kuwekeza hapo.” Dangote aliwaambiwa waandishi wa habari wa Harare.
Aliko Dangote na mwanae Halima kwenye sherehe ya Times 100 Gala jijini New York Marekani.Mipango mingine aliyonayo juu ya Zimbabwe ni pamoja na uwekezaji wa uchimbaji madini na uzalishaji wa umeme nchini humo. Kama serekali ya Zimbabwe ikitoa kibali basi ujenzi wa kiwanda hicho utanza mwaka 2016 na ujenzi utakapoisha kiwanda hicho kitakuwa kinazalisha tani milioni 1.5 za simenti kwa mwaka.

LEWIS HAMILTON NA RIHANNA NI WAPENZI!!!?

Dereva mahiri wa mbio za magari ya Formula 1, Lewis Hamilton amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Rihanna kwa zaidi ya mwezi sasa, toka zile picha za wao kuonekana pamoja katika tamasha linalofanyika kila mwaka Barbados ziingie katika vichwa vya habari, wengi wamekuwa wakiamini kuwa kuna kitu kinaendelea.
Hamilton na Rihanna wamekuwa karibu kwa muda sasa, kiasi kwamba watu wanaofuatilia nyendo za mastaa hao, wanahisi huenda wakawa wanatoka kimapenzi, kwani hakuna mmoja kati yao aliyekuwa ameweka wazi kama wako katika mahusiano ya kimapenzi au urafiki wa kawaida.
Hii ni moja kati ya picha zilizozua utata wa ukaribu wao katika tamasha Barbados
“Unajua nimefahamiana na Rihanna kwa kipindi kirefu kidogo, tumekuwa marafiki kwa muda mrefu wakati mwingine tumekuwa tukiongozana mara kwa mara” Alisema  Lewis Hamilton
Licha ya Lewis Hamilton ambaye amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi ya on-off na muimbaji Nicole Scherzinger kwa takribani miaka saba, anakanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rihanna.

HISTORI YA DROGBA SASA KITABUNI

Didier Drogba ni mmoja wa mastaa wakubwa Afrika na hata soka la Ulaya, Novemba mwaka huu (2015) anatarajia kuzindua kitabu kitakachozungumzia maisha yake kwa ujumla.
Akiwa na miaka yake 37 mshambuliaji huyo ameahidi kutoa kitabu hicho ambacho kitazungumzia pia na maisha yake akiwa Ufaransa, umuhimu wa elimu, jinsi ya kutafuta mafanikio katika maisha.
Pia kitazungumzia maisha yake ya kawaida na ya nje ya uwanja hasa akiwa na klabu yake ya Chelsea.