Akizungumza na Kituo cha Redio cha Sauti ya Marekani (VOA), Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Antipas Lissu amesema kuwa anashangaa sana maneno aliyoyasema jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema Dkt. Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi Januari, 2015 na mwezi Aprili, 2015 akathibitishwa na Kamati Kuu.
Akaendelea kusema ameshangaa Dkt. Slaa kusema Gwajima ndo alimleta Lowassa jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dkt. Slaa mwezi wa tano ndo alianza kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima.
Akasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 Julai, 2015 kwenye Kamati Kuu, Dkt. Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na Dkt. alilala kwenye gari.
Akasema Dkt. Slaa asiwadanganye Watanzania tatizo ni urais na mchumba wake na kwamba kama ameacha siasa tangu siku ya kikao cha Kamati Kuu alipoandika barua ya kujiuzulu kwa nini amepokea mshahara wa mwezi huu (Septemba, 2015)?
Kwanini anaendelea kutumia gari la chama la Katibu Mkuu na nyumba aliyonunuliwa na chama muulizeni awaambie kwanini anaendelea kunufaika na hayo yote toka CHADEMA?
No comments:
Post a Comment