DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 03, 2015

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUCHOCHEA MAENDELEO ENDELEVU NCHINI

Afisa wa Takwimu wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Emilian Karugendo akizungumza na waandishi habari katika warsha ya kuelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Ofisi ya Rais-Tume ya Mipango Lorah Madete akizungumza na waandishi wa habari juu ya jinsi ya mipango inavyotekelezwa na serikali katika kuelekea malengo 17 ya maendeleo endelevu iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Shule kuu ya uandishi wa habari, Dkt. Ayuob Rioba akizungumza na waandishi wa habari juu ya jinsi ya nafasi ya vyombo vya habari katika kushiriki katika malengo 17 ya maendeleo endelevu iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Vyombo vya habari vimetakiwa kushiriki katika maendeleo endelevu ya yenye malengo 17 yanayoanza 2016 hadi 2030 ili kuweza wananchi kufahamu kila lengo na kuweza kufikia mabadiliko chanya.
Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu yanatokana na kuisha kwa malengo ya milenia ambayo yamekamilika mwaka huu na kufanya nchi 88 duniani kukaa pamoja na kuja malengo hayo lengo likiwa ni kukamilisha malengo ya milenia ambayo yamekamilika mwaka huu pamoja na kuboresha sekta mbalimbali kupitia malengo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyoandaliwa na Hope Foundation for Social  Interprenuership, Mhadhiri wa Shule  Kuu ya Uandishi wa Habari  ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Ayub Rioba  amesema kuwa waandishi  wanawajibu kuelimisha wananchi kwa kila hatua ya melengo 17 ya maendeleo endelevu.
Rioba anasema baadhi ya nchi ikiwemo Singapore na Malaysia zimepiga hatua kubwa katika kutimiza malengo ya milenia inayokamilika kutokana na kuwashirikisha wananchi wake kupitia vyombo vya habari hivyo serikali na wadau wa masuala ya maendeleo wanatakiwa kufanya hivyo.
Mratibu  wa  Kanda ya Afrika  ya 2015,Steven Chacha amesema kama taasisi wamejipanga katika kuhakikisha wanashirikisha waandishi katika kuhakikisha malengo hayo yanayoangaliwa  katika kuleta mabadiliko yenye tija kwa wanananchi ambao wanatokana na changamoto.
Nae Afisa wa Takwimu wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS),Emilian Karugendo amesema kuwa NBS watafanya tathmini kutokana na viashiria hivyo katika kwenda katika malengo 17  ya maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment