Dereva mahiri wa mbio za magari ya Formula 1, Lewis Hamilton amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Rihanna kwa zaidi ya mwezi sasa, toka zile picha za wao kuonekana pamoja katika tamasha linalofanyika kila mwaka Barbados ziingie katika vichwa vya habari, wengi wamekuwa wakiamini kuwa kuna kitu kinaendelea.
Hamilton na Rihanna wamekuwa karibu kwa muda sasa, kiasi kwamba watu wanaofuatilia nyendo za mastaa hao, wanahisi huenda wakawa wanatoka kimapenzi, kwani hakuna mmoja kati yao aliyekuwa ameweka wazi kama wako katika mahusiano ya kimapenzi au urafiki wa kawaida.
|
No comments:
Post a Comment