DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 03, 2015

WAKALA JORGE MENDES NDIYE ANAYEVUNA FEDHA NYINGI BARANI ULAYA KIPINDI CHA USAJILI

Ikiwa ni siku moja toka dirisha la usajili lifungwe barani Ulaya, kila klabu inajiandaa kupiga mahesabu ni kiasi gani cha fedha imetumia kwa ajili ya kufanya usajili. Lakini wakati vilabu vikipiga hesabu ya kiasi gani imetoa na kuingiza wakati wa usajili, kuna mtu anaitwa Jorge Mendes yeye wakati huu, huwa anapiga hesabu ya kiasi alichoingiza.
Jorge akiwa na Radamel Falcao ni wakala wake pia
Jorge Mendes ni wakala maarufu ambaye anafanya shughuli hiyo kwa wachezaji kadhaa, huwa anatanguliza maslahi mbele kuliko kitu kingine chochote. Kati ya mwaka 2001 hadi 2010 amehusika kwa asilimia 68 katika kila usajili wa kuuza wachezaji kutoka vilabu vya BenficaPorto na Sporting Lisbon za Ureno.
Ni wakala wa Pepe pia
Mreno huyu kwa hizi siku za karibuni amekuwa anahusika kwa nafasi kubwa katika usajili unaofanywa na vilabu vya Atletico MadridDeportivo La CorunaMonaco na Valencia. Huyu ndiye wakala ambaye mara nyingi hufaidika katika uhamisho wa saa kadhaa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Haikuwa safari rahisi kwa Jorge Mendes kuwa wakala mkubwa wa wachezaji wa kubwa, safari ilianza mwaka 1996 kwa mteja wake wa kwanza Nuno walipo kutana katika Bar ya Guimaraes na kufanikisha uhamisho wa Nuno kwenda katika klabu ya DeportivoMendes ni wakala wa Cristiano Ronaldo na wachezaji wengine wengi.
Diego Costa ni moja kati ya wateja wa Mendes hiki ni kitu alichowahi kufanyiwa na Mendes katika masuala ya usajili.
“Jorge aliniambia natakiwa kupanda ndege na kwenda Madrid lakini nilikuwa sijui nini kinaendelea nilivyofika aliniambia alikuwa anasaini Atletico Madrid, baadae akaniambia kuwa tulikuwa katika nyumba ya Mkurugenzi wa Michezo wa Atletico Madrid  Jesús García Pitcarch nilikuwa simjui hata kidogo” alisema Diego Costa
Ameshawahi kusimamia uhamisho wa Luis NaniKama utakuwa unakumbuka vizuri Jorge Mendes ndiye wakala aliyepewa zawadi ya kisiwa  na Cristiano Ronaldo katika harusi yake, kupitia biashara hiyo katika kipindi cha miaka 20, Mendes anatajwa kuingiza kiasi cha poundi bilion 1 na anatajwa kama wakala ambaye mipango yake ya uhamisho mingi huwa inafanikiwa. Picha na habari kwa hisani ya millardayo.com

No comments:

Post a Comment