DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 03, 2015

TFF YATOA TAARIFA MCHEZO KATI YA TAIFA STARS Vs NIGERIA SEPTEMBA 5

Mkuu wa Idara ya Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania-TFFBaraka Kizuguto akiongea na Waandishi wa Habari leo. 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari wa shirikisho hilo, Baraka Kizuguto ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuelekea mchezo wa Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles mechi itakayopigwa jumamosi ya Seotemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
“Kocha amefurahi kuwapokea wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa na kwa hizi siku zilizo bakia, ana imani kabisa atafanya maelekezo ya mwisho na wachezaji wengine kuelekea mchezo huo, ana imani timu itafanya vizuri” alisema Kizuguto
Hata hivyo kwa upande wa timu ya taifa ya Nigeria bado haijatoa taarifa rasmi inakuja na msafara wa watu wangapi na muda itakao wasili Dar Es Salaam, ila kupitia kwa afisa habari wao ni kuwa timu itawasili Dar Es Salaam kwa ndege ya kukodi na kuna uwezekano wa kufika Dar Es Salaam saa 4 usiku Septemba 3. Waamuzi wa mchezo huo ni kutokea Rwanda watawasili Septemba 3. Muamuzi wa kati ni Luis Hakizimana wasaidizi ni Onole SimbaJean Bosco Tegeka na muamuzi wa akiba ni Abdul Karim Twagilamuzika na Charles Kasembe kutokea Uganda. Picha na habari ni kwa hisani ya millardayo.com.

No comments:

Post a Comment