DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, September 02, 2015

MAN U YAMSAJILI ANTHONY MARTIAL AKITOKEA AS MONACO YA LIGUE 1

Dakika zipatazo 40 kabla ya dirisha la usajili barani Ulaya kufungwa rasmi jana, Klabu ya Manchester United imetangaza usajili wa mshambuliaji mpya.
Mshambuliaji huyo ni Anthony Martial, kinda mwenye miaka 21, raia wa Ufaransa ambaye alikuwa akikipiga katika Klabu ya As Monaco ya Ligue 1.
United wamekuwa sokoni kutafuta mshambuliaji wa kumsaidia Wayne Rooney na kocha Louis Van Gaal aliahidi kusajili mshambuliaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa lakini haikutegemewa angemsaini kinda huyo kutoka Ufaransa.
Bei aliyonunuliwa mshambuliaji huyo bado haijawekwa wazi ila ripoti zinasema United wameilipa Monaco kiasi cha £36m.

No comments:

Post a Comment