DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, September 09, 2015

ABIRIA 159 WA NDEGE YA BRITISH AIRWAYS WANUSURIKA KIFO

Kama hii dharura ingetokea wakiwa katikati ya safari basi vyombo vya Habari Duniani vingekuwa na stori tofauti kabisa… Ndege ya Shirika la British Airways ilikuwa tayari kwa ajili ya safari kutoka Uwanja wa Ndege Las Vegas Marekani, ndani kulikuwa na abiria 159 pamoja na wahudumu wa Ndege 13.

Ajali hiyo ilitokea ghafla ambapo injini ya kushoto ilishika moto wakati ndege hiyo tayari ilikuwa kwenye njia ya kuruka… ikabidi safari iishie hapo na abiria wote watoke ndani ya Ndege kwa dharura.

Majeruhi ni wachache ambao walipata majeraha madogo madogo lakini hakuna taarifa ya mtu yoyote kufariki.

Muda mfupi baadae Rubani mmoja wa Ndege hiyo aliwaambia abiria hao kwamba ana uzoefu na kazi ya Urubani kwa muda mrefu lakini hakuwahi kupata tatizo la aina hiyo katika kazi yake, na chanzo cha moto huo ilikuwa ni tatizo la kiufundi kwenye injini ya Ndege hiyo.

No comments:

Post a Comment