DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, September 02, 2015

DK.SLAA ATANGAZA KUACHANA NA SIASA

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. Jana ameibuka na kusema  ya moyoni kuwa amejivua uanachama  rasmi wa chama cha CHADEMA pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama hicho na kuachana kabisa na siasa  kutokana na mambo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya chama chake hayakumridhisha na hakukubaliana nayo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndiyo maana ameamua kuachana na siasa  rasmi jana.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
Baadhi ya wananchi pamoja na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt.  Wilbroard Slaa jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment