DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, September 01, 2015

ALEX SONG ARUDI TENA KUKIPUTA WEST HAM UNITED

Agosti 31 na Septemba 1, 2015 ni siku ambazo habari nyingi za michezo barani Ulaya zitatawaliwa na vichwa vya habari za usajili, kwani dirisha la Usajili kwa Hispania na Ufaransa linaripotiwa kufungwa, lakini nchini Uingereza bado zimebaki saa kadhaa na wenyewe wafunge, klabu ya West Ham United imetumia vizuri saa hizo zilizosalia kumrudisha Alex Song.
West Ham United imefanikiwa kumrudisha kiungo wa kimataifa wa Cameroon aliyekuwa katika Klabu ya FC Barcelona ya Hispania Alex SongWest Ham wanamrudisha kiungo huyo baada ya kuitumikia kwa mkopo timu hiyo msimu uliyomalizika.
Song amerudi tena kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu hiyo akitokea FC Barcelona ya Hispania ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa wakati yupo Arsenal, kwani Song amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha FC Barcelona. Pamoja na hayo picha aliyoweka mtandaoni akiwa na Emmanuel Adebayor huenda pia mshambuliaji huyo wa Togo yupo njiani kujiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur.
Picha ya Song aliyoposti Instagram akiwa na wakala wake pamoja na Adebayor saa kadhaa baada ya kujiunga na West Ham. Picha kwa hisani ya millardayo.com

No comments:

Post a Comment