DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 03, 2015

MIILI YA WANAJESHI 12 WA UGANDA WALIOUAWA NA AL SHABAAB SOMALIA KUSAFIRISHWA LEO

Taarifa iliyonifikia ni kuhusu wanajeshi wa Uganda kuuawa na wapiganaji wa Al Shabaab, Somalia wakiwa kwenye kambi ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika AU.
Miili ya wanajeshi 12 inatarajiwa kusafirishwa wakati wowote kwenda Uganda kwa ajili ya maziko ya Kitaifa.
Wanajeshi wa Uganda ni miongoni mwa kikosi cha wanajeshi 22,000 cha AU, kinachokabiliana na wapiganaji hao kutoka Somalia.
Mmoja wa wanajeshi wa AU akiwa kazini.


Ripoti nyingine zinasema wanajeshi waliouawa kwenye uvamizi huo katika kambi yaJanale, kilomita 90 kutoka Kusini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, ni kati ya 20 hadi 50.
Wakazi wa eneo lililotokea shambulizi hilo zinasema shambulio hilo lilianza kwa shambulio la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwa kulipua gari lililotegwa bomu kwenye lango la kambi hiyo, na kisha kukawa na ufyatulianaji wa risasi uliodumu zaidi ya saa moja.

No comments:

Post a Comment