DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 03, 2015

DR. SHEIN AZINDUA MNARA WA KUMBUKUMBU ZANZIBAR JANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)  na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa Ujenzi wa Kampuni ya Habconsult Bw. Habid Nury anayohusiana na Ramani ua Ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya uzinduzi wa Mnara huo jana uliopo Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata Utepe kushiria Uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya miaka50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,sherehe za Uzinduzihuo ulifanyika jana katika viwanja vya Michenzani Mjini Unguja (katikati) Mke wa Rais Mama mwanamwema Shein na (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa ZSSF Nd,Mussa Yussuf akitoa maelezo kwa   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) wakati alipotembelea Chumba cha Filamu katika Mnara wa Kumbuklumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya uzinduzi rasmi uliofanyika jana katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati walipotembelea sehemu za mnara wa kumbukumbu baada ya uzinduzi uliofanyika   jana katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)naMkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na viongozi wengine wakati walipotembelea sehemu za mnara wa kumbukumbu baada ya uzinduzi uliofanyika   leo katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akiangalia darubini wakati alipopanda juu kabisa ya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia Mji wote wa Unguja baada ya kuuzindua rasmi leo katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee(kulia).
Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Abdulwakil Haji Hafidh katika sherehe za Uzinduzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50mya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar zilizofanyika leo katika Viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar. (Picha zote na Ikulu Zanzibar).

No comments:

Post a Comment