Memphis Depay wa Man United akiwa Uholanzi
Cristiano Ronaldo tayari yeye ameshajiunga na timu yake ya taifa ya Ureno na kuanza mazoezi. Timu ya taifa ya Ureno yenyewe itacheza mechi moja ya kirafiki siku ya Septemba 4 dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa kabla ya kusafiri kwenda kucheza mechi na Albania ya kuwania kufuzu Euro 2016.
Alex Sanchez naye amejiunga na timu yake ya taifa ya Chile kujiandaa na mechi za kimataifa za kirafiki ambazo zipo katika kalenda ya FIFA alipiga picha na kuweka katika mtandao wa twitter. Chile wataikaribisha Paraguay siku ya Jumamosi ya Septemba 5.
|
No comments:
Post a Comment