|
Baada ya Alex Song kujiunga na klabu ya West Ham United kwa mkopo wa muda mrefu, ni msimu wake wa pili kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo akitokea FC Barcelona ya Hispania, imethibitika kuwa winga wa kimataifa wa Nigeria Victor Moses amejiunga na West Ham kwa mkopo akitokea klabu ya Chelsea.
Moses ambaye alikuwa akitakiwa na klabu ya Tottenham Hotspur amekuwa mchezaji wa pili kwa mkopo kuwasili katika klabu ya West Ham United baada ya Song. Hii sio mara ya kwanza kwa klabu ya Chelsea kumtoa winga huyo kwa mkopo kwani misimu miwili nyuma walimtoa katika klabu ya Liverpool na baadae Stoke City na sasa West Ham.
Pamoja na hayo West Ham imemsajili Nikica Jelavic kutokea katika klabu ya Hull Citykwa mkataba wa miaka miwili.
|
Habari na picha ni kwa hisani ya millardayo.com
No comments:
Post a Comment