Muigizaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, Ramsey Nouah.
Muigizaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, Ramsey Nouah amekaririwa akisema kuwa, yuko tofauti kabisa na wasanii wenzake wa nchini humo wanaokimbilia kwenye siasa kila kukicha na kuongeza kuwa mashabiki wake wasitegemee Ramsey kujiunga na siasa.
Akifanyiwa mahojiano maalum na mtandao wa NET wa nchini humo, Ramsey alisema kuwa: ‘Sijui jinsi gani naweza kuwa mwanasiasa, mimi sio mwanadiplomasia kivile. Sijui namna ya kuyapangilia maneno yakafana kama wanasiasa wanavyoweza kufanya. Mimi siko hivyo’ Alisema Ramsey Nouah. Na NaijaGists.com
|
No comments:
Post a Comment