DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, September 01, 2015

JK AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NATIONAL DEFENCE HEADQUARTERS

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi muda mfupi baada ya kuwasili eneo la Lugalo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa National Defence Headquarters.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Makamanda wa Jeshi la Ulinzi wakati wa uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kitambaa wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,  Jenerali Davis Mwamunyange, Watatu kushoto ni Waziri wa Ulinzi Dkt. Huessein Ali Mwinyi na kulia ni Bwana Hu mwakilishi wa kampuni ya ujenzi kutoka China.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters Lugalo jijini Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimuonyesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mchoro wa majengo ya Makao Makuu ya Ulinzi yatakayojengwa eneo la Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Picha na Fred Maro. 

No comments:

Post a Comment