DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, September 01, 2015

YAELEZWA RELI YA KATI KUANZA KARABATIWA HIVI KARIBUNI

 Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya kuchukua hatua kubwa kuanza  kufufua reli ya kati. Sitta aliyasema hayo jana jiji  Dar es Salaam kuwa muda wowote, ujenzi wa reli hiyo utaanza ili kuongeza kasi ya maendeleo  nchini.
Waandishi wa habari walio hudhuria mkutano na Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta, wakimsikiliza kwa makini.
 (Picha na Emmanuel Mssaka).

Na JenikisaNdile –MaelezoSERIKALI  kwa kushirikiana na kampuni ya reli Asset holding imejizatiti kuimarisha miundo mbinu ya reli itakayogharimu shilingi Trilioni 16 katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samweli sitta amesema kuwa  mkakati ni kuimarisha  reli  katika maeneo mbalimbali  nchini.Aliongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na uboreshwaji wa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Songa Mpiji. Mtwara hadi Mbambabay, Songea hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.“Lengo  la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi  kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo  zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi “ amesema Mhe. Sitta.Aliongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa  ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.Aidha alibainisha kuwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya reli kutasaidia katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.


No comments:

Post a Comment