DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, September 01, 2015

MAELFU WAFURIKA UWANJA WA MAJI MAJI RUVUMA KUMSIKILIZA MAGUFULI!

Mgombea Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini  humo mkoani Ruvuma, Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka Kidato cha Nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya.

 Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dkt. Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma.
Dkt. Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Eng. Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi, ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUVUMA.










No comments:

Post a Comment