Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza imeonyesha muonekano wa uwanja wao mpya ambao hadi mwaka 2020 inaripotiwa kuwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa umekamilika. Bado mashauriano yanaendelea kuhusiana na wakazi wa eneo husika utakapojengwa uwanja huo.
Mpango wa mmiliki wa Klabu ya ChelseaRoman Abramovich ni kutumia poundi milioni 500 katika ujenzi wa uwanja huo ili uwe biashara tofauti inayojitegemea mbali na Chelsea. Ujenzi huo ambao unatarajiwa kuanza baada ya miezi 9 kutoka sasa utaifanya Klabu ya Chelsea kuhama uwanja wao wa Stamford Bridge na kutumia Uwanja wa Wembley kwa kipindi cha misimu mitatu.
Ujenzi huo wa Uwanja mpya wa Stamford Bridge utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 sawa na uwanja wa Taifa la Tanzania uliopo jijini Dar Es Salaam, ambapo uwanja wa sasa wa Chelsea unachukua watu wasio zidi 41,000.
Huu ni muonekano wa sasa wa Uwanja wa Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment