Ni utaratibu ulioanza mwaka 2014 kwa kampuni ya Multichoice kukutana na Waandishi wa habari/Watangazaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuonyesha na kuyazungumzia kwa upana vipindi na mengine mengi yanayopatikana kupitia bidhaa yake ya DStv.
Tamasha hili linafanyika kwa wiki nzima kwenye kisiwa cha Mauritius kuanzia September 1 -6 likiitwa MultiChoice Africa Content Showcase Extravaganza ambalo mwaka huu limehudhuriwa na Waandishi mbalimbali wakiwemo wa Tanzania pamoja na mastaa kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Genevieve Nnaji, Ramsey Noah na Mr. Flavour wa Nigeria.
|
No comments:
Post a Comment